Showing posts with label POLITICAL NEWS. Show all posts
Showing posts with label POLITICAL NEWS. Show all posts
Mange Kimambi Awachana Wabunge wa Upinzani
Upinzani punguzeni Jazba ...Mnajikweza Sasa.. Sijui Bashite kawaloga... Speaker angekaa kimya kwenye hili ndo yangekuwa yale Yale ya double standards tunayoyakataa kwa Rais Magufool na Bashite... Kama Bashite anashughulikiwa kwa kulidhalilisha bunge kwa kusema wabunge wanalala tu Inabidi Hata nyinyi mliheshimu Bunge...Bashite aliitwa mbele ya kamati ya maadili na alifika why nyinyi mgome? Hatutaki double standards Jamani!!!!Hata kama hamkupenda maamuzi yake hamtakiwi kumtukana speaker.. nendeni Jamani bila kukamatwa mlimalize hili ili tuendelee na Bashite mbona mnaunguza picha sasa? Haki mganga wa Bashite kibokoooooo... Badala ya kumshighulikia Bashite Bunge limebaki kutifuana wenyewe kwa wenyewe... So stupid! 😏😏 .
.
Huyu spika amekuwa very fair kwa wabunge woote, msimtibue tafadhali. Mdee umemkosea sana spika huwezi kumwita fala aiseeeee. Especially spika kama Ndugai....Na ukweli inabidi usemwe, tatizo haikuwa wagombea wenu tatizo ni Chadema hakuna demokrasia ya kweli, sio kwenye viti maalum sio kwenye nini.. You guys have to change!! Period!
.
.
Ushauri wangu kwa WaBunge Wa upinzani hayo mambo ya kutoa lugha kali yanawaharibia mnooo. Muache mara moja.Nyinyi ni wabunge, lugha chafu tuachieni sisi tulioko kitaa. .
Makonda afunguka Kuhusu Wasanii..Atoa Amri Nyingine Mpya..!!!
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amepiga marufuku  uuzwaji, uingizwaji wa filamu za nje ambazo hazina stika za TRA ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha amesema baada ya siku kumi ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa wamekiuka agizo hilo.
Amesema hayo amapema jana ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kutembelewa na wasanii wa filamu wakiongozwa na Jacob Stephan wakilalamikia kuzagaa kwa kazi zao ambazo zimedurufiwa na wafanyabishara wasiowaaminifu.
Akiongea na waandishi pamoja na wasanii hao, Mh Makonda aliwaagiza watu wa bodi ya filamu kufanya tadhmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi yanayouza mikanda ya filamu jiji Dar es Salaam.
Wasanii hao pamoja na wasambazaji walidai hawanufaiki na kazi zao za filamu kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridha yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato.
Wasanii wengine ambao walifika ofisini hapo ni pamoja na Ray Kigosi, Odama, Tino, Jimmy Mafufu pamoja na wasambazaji wa filamu.

Babu Tale Amshukia Paul Makonda..Adai yeye Ndo Mwenye Jukumu la Kujua Roma Yupo Wapi

Uoga ni uzembe me nazani mwenye jukumu la kujua Roma yupo wapi ni Mkuu wa koa sababu yeye ndio kiongozi wa kamati ya usalama ya mkoa sasa ikiwa tumezunguka vituo vyote vya polisi na mwenzetu atumuoni nani wa kumfuata kumwambia tunamtaka mwenzetu kama sio @paulmakonda me naanza hili bila uoga mkuu wa mkoa naomba utusaidie kutuambia mwenzetu @roma2030 alipo. Tukutane Tongwe mida hii me nipo kwa foleni wakuu #uogauzembe#freeroma
TANZIA: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia

TANZIA: Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia.

SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS
​
Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.

Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.

Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.

Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.

Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.

Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.

Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.

Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.

“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.

Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.

Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.

Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.

Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.

Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.

Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Kanuni za Freemason zinafundisha nini?

Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.

“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.

Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki.

Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.

“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:

“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.

Chanzo: Mwananchi
Spika wa Bunge ameagiza kukamatwa Mbunge Halima Mdee

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.
Mwakyembe asema hawezi kulifumbia macho tukio la kuvamiwa clouds

Dk. Mwakyembe aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, muda mfupi baada ya Spika wa Bunge kusitisha shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria hadi leo saa 3:00 asubuhi.

Nipashe ilitaka kujua kinachoendelea kuhusu uchunguzi dhidi ya Makonda ambaye kamati ya watu watano iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ilitoa ripoti ikidai Mkuu wa Mkoa huyo alivamia kituo cha TV cha Clouds akiwa na askari wenye bunduki na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa kituo hicho.

Kamati hiyo ilidai kubaini Makonda alifanya hivyo ili kulazimisha video ya mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, irushwe hewani.

Katika majibu yake, Dk. Mwakyembe alisema suala hilo ni “zito” na haliwezi kuachwa lipite bila kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Huku akiendelea kuikosoa ripoti ya kamati ya Nape ambayo amekuwa akisisitiza haijakidhi matakwa ya kikatiba na kisheria kwa kushindwa kumhoji Makonda, Dk. Mwakyembe alisema Mkuu wa Mkoa huyo atahojiwa kwa mambo tisa yanayohusiana na tukio hilo.

“Hili ni suala zito maana linahusisha uvamizi ambao ni kesi ya jinai,” alisema Mwakyembe ambaye ni daktari wa sheria na Waziri wa Katiba na Sheria mpaka wiki mbili zilizopita.

“Kuna vitu tisa ambavyo upande wa pili (Makonda) utaulizwa.”

Dk. Mwakyembe hata hivyo, alikataa kuvitaja vitu hivyo tisa huku akisita pia kutaja tarehe ambayo Makonda atahojiwa.

“Upande wa kwanza (Clouds TV) tayari umeshahojiwa na ripoti tunayo. Upande wa pili nao tutauhoji na wenyewe pengine una hoja,” alisema Dk. Mwakyembe.

“Ili kukidhi matakwa ya kikatiba na kisheria, ni lazima tuuhoji upande wa pili. Hili suala kama nilivyotangulia kusema ni la jinai. Lazima mtuhumiwa apate haki ya kujitetea.
“Ukifika mahakamani, hata yule mwenye kesi ya mauaji lazima tumpatie wakili, hata kama tunao uthibitisho kwamba ameua.”

Machi 29, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari alipokaribishwa ofisi kwake mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe alisema hawezi kuikabidhi kwa wakubwa wake ripoti hiyo ya kamati ya Nape bila kuwapo na maelezo ya Makonda.

“Taaluma yangu ni sheria, hivyo siwezi kufanya jambo hilo la kupeleka malalamiko ya upande mmoja kwa mabosi zangu bila kusikiliza ule mwingine,” alisema Mwakyembe siku hiyo.

Alisema hatateua kamati nyingine ya kufuatilia jambo hilo, bali yeye na viongozi wenzake watakuwa kamati hiyo ili kuuhoji upande wa pili kisha kupeleka taarifa kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais mwenyewe.

JELA MIEZI SITA
Kamati ya watu watano iliyoundwa na Nape kuchunguza tukio la uvamizi wa televisheni ya Clouds ilibaini kuwa kiongozi huyo aliwatishia kuwafunga jela miezi sita wafanyakazi wake endapo wasingerusha kipindi alichokitaka.

Pia Kamati hiyo ilibaini Makonda aliwatisha kuwa angewaingiza wafanyakazi hao kwenye tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya kama wasingerusha kipindi chake.

Aidha, kamati ilibaini kuwa Makonda aliwatisha wafanyakazi wa kituo hicho ili wasitoe taarifa za uvamizi wake, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Katibu wa Kamati hiyo, Deodatus Balile.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Dk. Hassan Abass, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, ni Mhariri Mkuu wa Magazeti ya The Guardian, Jesse Kwayu, Nengida Johannes wa Upendo Media na Mabel Masasi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ilidaiwa Makonda akiwa na askari kadhaa wenye bunduki, alivamia kituo hicho na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha ‘Da Wikend Show’ kurusha taarifa ya mama anayedai kuzaa na askofu Gwajima, bila ya kiongozi huyo wa kidini kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Ingawa taarifa ni ya upande mmoja, kwa mujibu wa Balile mtuhumiwa alikubali kuwaona, lakini wakati wakipanda ngazi kwenda ghorofani iliko ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala jijini, Makonda aliteremka kwa kutokea mlango wa nyuma.
Mzee Mwinyi Afunguka Kuhusu Tanzania ya Magufuli.

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi amemuomba kiongozi wa dini ya Wahindu ya Swaminarayan Duniani, Mahant Swami Maharaji kuiombea Tanzania amani na umoja viweze kudumu na kusiwepo aina yoyote ya ubaguzi kwa sasa na hata vizazi vijavyo.
Mwinyi aliyasema hayo Dar es Salaam baada ya kualikwa katika hafla ya kumkaribisha kiongozi huyo hapa nchini na kukutana na waumini wa dini hiyo.
Pia ilikua ni maadhimisho ya miaka 40 tangu kujengwa misikiti miwili ya dini hiyo hapa nchini.
Alishukuru kwa kualikwa katika hafla hiyo ya kidini kwani sio jambo la kawaida kupokea ugeni wa kiongozi wa kidini nchini.
“Sina shaka kuwa sio nchi zote wenye kuwa na uwezo wa kumuona kiongozi mwenye nafasi kubwa kama hiyo katika nchi zote,” alisema na kuongeza kuwa kama Watanzania wengine amekuwa mwenye bahati.
Alimkaribisha kiongozi huyo nchini na kumtaka kuiombea sana Tanzania ili iendelee kudumisha amani na umoja na licha ya kutokuwepo kwa aina yoyote ya ubaguzi, aendelee kuomba ili hali hiyo isiwepo kamwe na wananchi waendelee kuishi kama ndugu.
Kwa upande wake, kiongozi huyo ambaye ni wa sita kwa nafasi hiyo, Maharaji alisema ataendelea kuiombea Tanzania na dunia nzima kwa ujumla ili wananchi wake waendelee kubarikiwa katika maisha yao pamoja na kukuza maendeleo yao.
Alisema mwanadamu siku zote hupenda raha lakini ni vyema wakafahamu kuwa hakuna raha kubwa kama kupata kutoka kwa Mungu kwa kuwa raha nyingine zote ni za muda, hazidumu.
“ Starehe ya mwanadamu ni ya muda mfupi na raha ya kuishi anayeitoa ni Mungu na ambayo haidumu, hivyo siku zote yapasa kuomba sana kwa Mungu kupata raha ya kudumu,” alisema na kusisitiza wajibu wa kila mwanadamu kuomba amani siku zote na kila wakati na kuishi kwa kanuni za Mungu.
Mama Samia Suluhu Hassan Awaumbua Kina Mange Kimambi na Genge Lake..Afunguka Haya Kuhusu Uwekezaji Nchini

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Tanzania ni moja ya nchi salama kwa uwekezaji Afrika.
Amesema hilo linasababishwa na kutokuwa na matatizo ya migogoro ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa mali za wawekezaji ikilinganishwa na nchi zingine Afrika.
Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua maonesho ya kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika Dar es Salaam.
Pia alikaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Ufaransa kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa kwenye kilimo, nishati, utalii na usafiri kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.
Makamu wa Rais alisema maonesho hayo ambayo yataambatana na kongamano la kibiashara la nchi hizo mbili ni fursa ya kipekee kwa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa kubadilishana uzoefu katika masuala ya kibiashara na uwekezaji.
Alieleza kuwa katika kuelekea kwenye uchumi wa viwanda Tanzania haiwezi kufanya kazi hiyo peke yake, bali kwa kushirikiana na mataifa makubwa yenye teknolojia ya kisasa katika uwekezaji ikiwamo Ufaransa.
Aliwahakikishia wawekezaji wote wanaokuja nchini kuwa Serikali itafanya kila linalowezekana kuendelea kujenga mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji.
Alisema ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji Afrika, Serikali imeendelea kutenga bajeti ya kutosha kuimarisha miundombinu ya bandari, reli, barabara, usafiri wa anga ili kurahisisha usafiri na usafirishaji nchini.
Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili kwa kina fursa za uwekezaji nchini hasa kwenye nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano na miradi ya maendeleo.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram,Mara Kadhaa Mwanadada Mange Kimambi Amekuwa Akidai kuwa Tanzania si Sehemu Salama kwa Uwekezaji kutokana na aina ya Serikali Iliyopo hivi sasa.
Kwa hili la Halima Mdee kumtusi Spika, Tunakoelekea ni Kubaya zaidi
Nadhan hapa tunapasa kuweka itikadi zetu za vyama ,dini na kabila pembeni. kuna kipindi tunapaswa kusimama kama watanzania tukaweka mambo mengine yote mifukoni mwetu tukabaki na utanzania.

Tanzania ya sasa si tanzania ya jana...inabadilika inakuja na mambo leo ambayo mengine si mazuri. Nimemsikia mbunge mmoja akiongea lugha ya ajabu sana bungeni ambayo sitegemei mbunge msomi na ampambanaji ongee hata kama alikwazika sana. Angalau kistaarabu angeomba msamaha maana wanasema ada ya mja hunena uungwana ni vitendo.

Kwa mbunge kutamka maneno "fala" "mpumbavu" si maneno mazuri ingawa sishangai hili tatizo si kwa wabunge vijana tu . tulishawah sikia mtu mzima mmoja akiitwa wenzie "wapumbavu" si maneno ya kistaarabu tukiacha ashakum si matusi. Kuna lugha za mitaani hizo zisipelekwe bungeni kwa nini wabunge huwa hawapewe semina ya communication skills? maneno kama "kimenuka" "fala", "wapumbavu" hatutegemei kuyasikia bungeni.

Wapumbavu wote basi wanapotamkwa watamkwe pia na huo upumbavu walioufanya au nena wasiishiwe kuitwa wapumbavu. Nimesikitika sana kwa aina hii ya wabunge  ni wapi tulipokosea sisi watanzania?


Najua bado kuna watu watakuja kutukana hapa na kumtetea.Kudhihirisha kuwa tuna taifa ambalo either limeathirika na viroba au matumizi ya bangi lakini sisi wenye akili timamu hatutanyamaza.
Sanamu ya Mwl. Nyerere yazidi kupata umaarufu.
SANAMU ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Nyerere Square mjini hapa, imepata umaarufu kutokana na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali mchini kufika na kupiga picha za kumbukumbu na sanamu hiyo.
Sanamu hiyo ya Mwalimu Nyerere ambayo Baba wa Taifa ameshika fimbo mkononi, ipo mjini Dodoma, inatumiwa na watu mbalimbali kupiga picha za kumbukumbu mbalimbali kutokana na heshima ya kiongozi huyo.
“Watu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa Dodoma na mikoa mingine wanaofika Dodoma wanakwenda mahali hapo na kupiga picha za kumbukumbu mbele ya sanamu hiyo ya Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere,” anasema Masoud Abdallah ambaye ni mpigapicha katika eneo hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Hilda Meada katika mazungumzo na gazeti hili, alisema eneo la Nyerere Square ambalo ni maarufu kwa wapigapicha ni miongoni mwa maeneo ambayo CDA imeyakabidhi kwa manispaa.
“Eneo hilo ambalo lilikuwa likisimamiwa na kufanyiwa ukarabati na uboreshaji na CDA na sasa limekabidhiwa kwa Manispaa ya Dodoma ambayo inajipanga kuhakikisha eneo hilo na mengine yaliyopo Dodoma yanaboreshwa na kulingana na mji huu kuwa makao makuu ya serikali,” alisema Maeda.
Alisema manispaa ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha eneo hilo na maeneo mengine ya wazi yanafanyiwa ukarabati na uboreshaji wa kutosha ili kuendana na hadhi ya mji.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema manispaa imejipanga kikamilifu kuhakikisha maeneo yaliyokuwa ya wazi ambayo yamerudishwa kutoka CDA wanataka kuyaboresha na kuhakikisha yanakuwa sehemu ya vivutio muhimu kwa watu mbalimbali wanaotembelea likiwamo hilo na Nyerere Square.
Mpigapicha Said Juma alisema, hicho ni kituo chao kutokana na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini kufika hapo na kutaka kupiga picha na sanamu ya Baba wa Taifa.
“Hapa kimekuwa kituo chetu cha kupigia picha kutokana na watu wengi wanaotoka mjini Dodoma, kuja kuweka kumbukumbu ya kuingia hapa kwa kupigia picha mahali hapa,” alisema Juma.
Hatukubaliani na Matokeo na Tutakwenda Mahakamani’ -Freeman Mbowe

April 5, 2017 Bunge limepiga kura za kuwapitisha wawakilishi wa bunge la Afrika Mashariki ambapo wagombea saba pekee ndio waliopitishwa kwa kupigiwa kura za ndio huku sita kati yao wakitokea Chama cha mapinduzi (CCM) na mmoja Chama cha wananchi CUF huku wagombea wawili wa CHADEMA wakikosa sifa baada ya kupigiwa kura nyingi za HAPANA.

Nje ya ukumbi wa Bunge Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe ameongea na waandishi wa habari na kusema kuwa hawakubaliani na matokeo na watakwenda Mahakamani.

Matokeo ya Bunge la Afrika Mashariki: Saba Washinda Wagombea wa CHADEMA Waangukia Pua
MATOKEO YA UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI



KUNDI A: WANAWAKE

1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM - KURA 196

2. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM - KURA 197

3. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM - KURA 125

4. Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA - KE - CCM - KURA 137

KUNDI B: ZANZIBAR

1. Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME ME CCM - KURA 254

2. Ndg. Maryam Ussi YAHYA KE CCM - KURA 195

3. Ndg. Mohamed Yusuf NUH ME CCM - KURA 65

4. Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI KE CCM - KURA 142

KUNDI C: VYAMA VYA UPINZANI

CHADEMA

1. Ndg. Ezekia Dibogo WENJE - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIYO 124 HAPANA 174

2. Ndg. Lawrence Kego MASHA - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIO 126 HAPANA 198

CUF

1. Ndg. Habibu Mohamed MNYAA - ME - CUF KURA 188

2. Ndg. Sonia Jumaa MAGOGO - KE - CUF KURA 06

3. Ndg. Thomas D.C MALIMA - ME - CUF- ALIJIONDOA

4. Ndg. Twaha Issa TASLIMA - ME - CUF KURA 140

KUNDI D: TANZANIA BARA

1.Ndg. Adam Omai KIMBISA - ME - CCM 266

2. Ndg. Anamringi Issay MACHA - ME - CCM 23

3. Ndg. Charles Makongoro NYERERE - ME - CCM 81

4. Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE - ME - CCM 287

Wabunge saba ndio wamechaguliwa na nafasi mbili za CHADEMA bado zipo wazi.

WALIOSHINDA NI;

1. Fancy Haji Nkuhi

2. Happiness Elias Lugiko

3. Abdallah Hasnu Makame

4. Maryam Ussi Yahya

5. Habibu Mohamed Mnyaa

6. Ngwaru Jumanne Magembe

7. Adam Omary Kimbisa
Zitto Kabwe Afunguka Uteuzi Uliofanywa na Rais Magufuli
KIONGOZI Mkuu wa Chama ACT- Wazalendo Zitto Kabwe aunga mkono uteuzi wa Mshauri wa Chama hicho Professa Kitila Mkumbo uliofanywa na Rais w John Magufuli.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoituma kwa vyombo vya habari  mchana huu akiwa Dodoma amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa mzalendo kwa kufanya uteuzi bila kujali itikadi ya Professa Mkumbo

 “Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kw mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na uzalendo wa kutumikia nchi yetu” ameeleza zitto.

Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya Chama ikiwemo Kamati Kuu. Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu kama mshauri wa chama. Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Taifa utokanao na kila mwananchi, ndio msingi wa kaulimbiu yetu ya 'Taifa Kwanza, Leo na Kesho', hivyo basi tunamtakia kila la kheri ndugu Kitila katika utumishi wake kwa Taifa letu katika nafasi yake hii mpya. Wizara Hii ni kubwa na muhimu Sana kwa nchi yetu. Maji ni tatizo moja kubwa ambalo wananchi wetu wanakumbana nalo na Kama Taifa hatujaweza kulimaliza. Tunamtakia kila la kheri ndugu Mkumbo katika kuongeza nguvu kumaliza kero ya maji na kuhakikisha tunaimarisha Kilimo cha Umwagiliaji nchi nzima. Tunamsihi aanze na ajenda ya Mfuko wa Maji Vijijini na kuanzishwa Kwa Wakala wa Maji Vijijini utakaosimamia upatikanaji wa Maji Kwa wananchi wetu.

Kwa hatua hii, tunaona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu Kwa kufanya kazi na watu wote bila kuwabagua Kwa itikadi zao za vyama. Watanzania ni wamoja na kauli za kuwagawa zinaumiza zaidi Taifa kuliko kuliweka pamoja. Tunaamini kuwa Rais Ana nia njema katika uteuzi huu na sisi tumempa baraka zote Mwanachama wetu mwanzilishi wa Chama kwenda kwenye nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma. Tunaamini hatamwangusha Rais na muhimu zaidi hatawaangusha Watanzania.
Jakaya Kikwete 'Zamu Yangu Kumuunga Mkono Mke Wangu'

Dkt Kikwete: Zamu yangu kumuunga mkono mke wangu

Rais Mstaafu wa awamu wa nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema ameshuhudia kiapo cha Mke wake, Mama Salma Kikwete baada ya kuteuliwa hivi karibuni kuwa mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Rais huyo mstaafu alifuatana na baadhi ya familia yake na kushuhudia mkewe akila kiapo hicho katika bunge lililoanza leo mjini Dodoma huku akisema kuwa ni zamu yake sasa kumuunga mkono mkewe.

“Leo asubuhi nimeshuhudia kiapo cha Mke wangu Mhe. Salma Rashid Kikwete kuwa Mbunge wa Kuteuliwa Bungeni Dodoma.Ni zamu yangu kumuunga mkono,” ameandika Dkt Kikwete kupitia akaunti yake ya Twitter.

Dkt Kikwete aliingia ndani ya bunge akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa bunge hilo.
Uteuzi wa Magufuli Utaniziba Mdomo-Semakafu
Mwanaharakati wa masuala ya jinsia nchini Tanzania Dkt. Avemaria Semakafu amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu huku akiweka wazi kuwa uteuzi huo utamfanya awe kimya katika harakati zake.

Akizungumza  ya simu mara baada ya uteuzi huo kutangazwa, Semakafu ambaye pia ni Mhadhiri Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uaminifu na uadilifu mkubwa, na kwamba kwa nafasi hiyo ni vigumu kuendelea kupigia kelele masuala mbalimbali kama alivyokuwa anafanya kwa kuwa nafasi hiyo ina utaratibu wake.

"Sasa hamtanisikia tena, ndiyo nimefungwa mdomo, huku huwa hawaruhusu kuongea". Amesema Dkt. Semakafu.

Dkt. Semakafu anafahamika zaidi nchini kwa kutoa na kuchangia mada mbalimbali kupitia mihadhara na vipindi vya luninga vinavyohusu mijadala mbalimbali ya kijamii na kitaifa. Pia alikuwa ni mjumbe katika Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014, wakati huo akiwa mratibu wa Mtandao wa wanawake na Katiba (Ulingo)

Kuhusu kuendeleza harakati zake, amesema ni vigumu kuzifanya harakati za jinsia lakini atajitahidi kutumia uwezo wake kusukuma masuala kadhaa yahusuyo elimu kwa mtoto wa kike kwa ushirikiano na watu atakaowakuta wizarani, lakini pia kwa kufuata miongozo iliyopo.

"Kwenda wizara ya elimu ni fursa kwangu lakini ifahamike kuwa nakwenda mahali ambapo tayari kuna mipango ambayo tayari imeshawekwa, kwahiyo ni kwenda kuangalia changamoto ambazo zimeanishwa na mipango iliyowekwa  na jinsi gani itatekelezeka katika kushughulikia kuzitatua... Nitakwenda kujifunza na kwa kutumia harakati zangu, waliopo pale pia watajifunza kwangu" Amesema Semakafu
Baada ya Zitto Kumpongeza JPM kwa Kumteua Kitila..Mange Kimambi Aja na hii.
Aisee Zitto unazingua .... Yani umeongea kama msemaji wa Ikulu sio opposition!! Seriously naomba ukajisikilize Tena kwenye Hii clip Yani umesound kama publicist wa Magufuli.... So sad yani 😭😩....Ndo maana hukutia mguuu clouds?? 😳😳 Nyie ndo tunawategea mkamwajibishe Rais kwa utumishi mbovu Alafu unakuja kumlamba lamba na kumsifia Hapa? 😳😳.. Aisee upinzani uko South Africa tu kwa kina Malema huku kwetu bado sana!!! #LipumbaJR
.
.
Magufuli alichokifanya Hapa ni kuwatenganisha upinzani... Na wewe umemruhusu afanye hicho kitu...... Yani in short umemsaidia Magufuli kudhoofisha upinzani. Kweli Zitto unasema Rais anaondoka kwenye kutenganisha watu, hivi ni kwamba huoni nchi ilivyotenganika kwa Sasa sababu ya Bashite? Very disappointed Na Huyu mtu! Yani I always thought Chadema ndo walimkosea huyu kaka Ila dah huyu jamaa mbaya kushinda Lipumba! Yani Zitto sio mtu!!!!
.
.
.
Na hamuwezi kuelewa why naongea Hivi, Jamani mimi kuna mtu wa CCM aliniapia Miungu yooooote just a few months ago wakati namposti posti Zitto kama opposer wa Magu..akaniambia wewe achana Na Zitto kabisaaa humjui na wala you don't know how the system works. Hapo Zitto anapiga kelele anatafuta pakumshikia Magu akipapata utamuona atakavyobadilika kama sio yeye... anatafuta pa kumshikia Magu kama alivyomshikaga JK mpaka wakamake a deal akaacha kuichokonoa serikali ya JK.Same thing Na Magu hapo anampa Magu jamba jamba mpaka Magu aingie line Alafu atatulia ataacha kuichonoa serikali kwa issue nzito Yani atabaki kama vile anagusia gusia tuu Ila sio ile kumu-Attack full kama mwanzoni.... Leo kanichekaaaa mnoooooo ananiambia haya mama much know umeona eeeeh??? Wewe bado mtoto mdogo huijui system sisi ndo tunaijua system, Doh, limenishuka shuuuu! Maana nilivyokuwa namtetea Zitto utasema nna undugu nae!!!
JPM amefanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 04 Aprili, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Prof. Kitila Alexander Mkumbo anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.

Kabla ya Uteuzi huu Prof. Kitila Alexander Mkumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Leonard Akwilapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarishi amehamishwa na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).

Bi. Maimuna Tarishi anachukua nafasi iliyoachwa na Mussa Uledi ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambako anajaza nafasi iliyoachwa na Dkt. Leonard Akwilapo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Ave Maria Semakafu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Wateule hao wataapishwa kesho tarehe 05 Aprili, 2017 saa 3:00 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Cuf ya Prof Lipumba Yazidi Kumdhalilisha Maalim Seif.
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtaka Maalim Seif Sharif Hamad kueleza ukweli ili jamii ipate kuelewa kinachoendelea ndani ya chama hicho hasa kuhusu mambo muhimu.
Hayo ni pamoja na suala la nafasi yake ya ukatibu mkuu kukaimiwa, Bodi ya Wadhamini na kesi nne mahakamani, ambazo Seif na wenzake walifungua.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya jana ilieleza kwamba anachofanya Maalim Seif na wenzake ni kuwatoa wana CUF kwenye hoja za kikatiba za kushughulikia mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho.
Kuhusu suala la kukaimiwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu, Sakaya alisema hilo ni  suala la kikatiba na si utashi wake au wafuasi wake.
"Tumeeleza na kunukuu ibara ya 93 kifungu cha 2 mara kadhaa. Kifungu hiki kinampa madaraka Naibu Katibu Mkuu anayetoka upande wa pili wa Muungano tofauti na anaotoka Katibu Mkuu, kukaimu nafasi na kutekeleza majukumu ya Katibu Mkuu mpaka pale Katibu Mkuu atakapokuwa tayari kutekeleza majukumu yake," ilisema taarifa hiyo ikimnukuu Sakaya.
Alisema anachopaswa kufanya Maalim Seif ni kusema kifungu hicho hakipo au hakisemi hivyo, ili jamii ipate kuelewa na si kubadilisha maneno.
“Ni kweli CUF tumeandika barua kumjulisha Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu suala hilo naye amejibu akikiri kupokea barua na ameridhia kwa mujibu wa Katiba yetu,” alisema.
Alisema Profesa Lipumba na Maalim Seif hakuna kati yao mwenye uwezo wa kumsimamisha mwenziwe au kuteua mtu wa kukaimu nafasi ya mwenziwe na kwamba suala la Maalim Seif kuomba kusajili Bodi mpya, na nakala ya maombi hayo kuyawasilisha Ofisi ya Msajili ni kichekesho kama si kujichanganya.
"Maalim Seif na genge lake wamefungua kesi Mahakama Kuu ya kutotambua msimamo na ushauri wa Msajili kuhusu uliokuwa mgogoro wa uongozi ndani ya CUF na inaitaka Mahakama Kuu itamke kuwa Msajili wa Vyama hana haki ya kuangalia mambo ya ndani ya CUF.
“Swali kwa Maalim Seif na genge lake,  je wanapopeleka nakala ya maombi ya kusajiliwa Bodi yao Ofisi ya Msajili huko si kuingilia mambo ya ndani ya vikao vya chama ? Au ndio kusema kwamba sasa Seif na genge lake wameamua kumtambua Msajili kupitia nyuma ya pazia?”
Aliongeza kuwa lingekuwa jambo jema kama Maalim Seif sasa angekiri wazi kwamba chama hicho kikatiba hakina Bodi halali kama ambavyo Msajili alisema kwamba Bodi ya Wadhamini ya CUF ni mfu na haipo kisheria, ndiyo maana sasa anahangaika kusajili Bodi mpya.
Alihoji kama hivyo ndivyo, je Maalim Seif anaweza kuieleza jamii na wana CUF kwa ujumla kuwa zile kesi nne mahakamani zilifunguliwa na Bodi ipi ikiwa hivi sasa yeye anaomba kusajili Bodi mpya? Au ndiyo kusema ameamua kufuta kesi zote kimyakimya?
Aliongeza kuwa ni vema akasema wazi ikiwa maombi yake ya kufungua Bodi mpya yatakubalika na kueleza ni ipi sasa itasimamia kesi mahakamani.  
"Maalim Seif hajui atendalo kwa sasa, ni vyema amwache Kaimu Katibu Mkuu Sakaya na Kamati mpya ya Utendaji wasimamie shughuli za chama ikiwamo ya kuwafanyia kampeni na kuwaombea kura wagombea wetu wa Bunge la Afrika Mashariki  na Kaimu Katibu Mkuu yuko Dodoma akifanya kampeni kwa wagombea wetu Habib Mnyaa, Thomas Malima na Sonia Magogo,” alisisitiza.
Aliwajulisha wana CUF kokote waliko na Watanzania kwa jumla yao kuwa chama hicho kiko katika mikono salama ya viongozi wanaojitambua ambao hawaendeshwi kwa fedha za kifisadi, bali wanaendesha chama kwa mujibu wa Katiba yake ya mwaka 1992 toleo la 2014.
kwa mara ya kwanza Nape auliza haya kama mbunge.
Kwa mara ya kwanza aliyekuwa Waziri wa habari Nape Moses Mnauye asimama bungeni kama mbunge na kuuliza swali kwa waziri wa uchukuzi na mawasilioano.

Nape Mnauye alisimama kuuliza swali la nyongeza ambapo aliitaka serikali kuweka mipango yao ya kufanya upanuzi wa Barabara na Reli.

Nape alitaka Serikali ielekeze mipango yao mapema katika upanuzi wa miundombinu iliyokaribu na makazi ya wananchi na kutowaweka wananchi njia panda katika kuyaeneleza makazi yao.
Akitoa mfano jimboni kwake Mtama amesema kuwa wananchi wapo njia panda kujua hatma yao.

Swali hilo lilijibiwa  na Naibu wa Waziri wa wizara hiyo Mhandisi Edwin Ngonyani wizara ya Uchukuzi na Mawasilioa na Kujibiwa na naibu Waziri wa wizara hiyo
 Waziri Ngonyani alijibu kuwa  Serikali imeweka alama kutoka mita 30 za kila upande wa barabara kuonesha hifadhi ya barabara
Wabunge CCM Wameitaka Serikali Kutoa Majibu Sahihi Bungeni kuhusu Utambulisho wa Mtu Aitwaye Daudi Bashite
Dodoma.  Wabunge wa CCM wameitaka Serikali kutoa majibu sahihi bungeni kuhusu utambulisho wa mtu aitwaye Daudi Bashite.

Sakata hilo liliibuka juzi katika kikao cha wabunge wa CCM kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini hapa.

Wabunge tofauti waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa, suala hilo lilihojiwa kwenye kikao hicho cha ndani ambacho hufanyika kabla ya mkutano wa Bunge kwa ajili ya kuwekana sawa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao walidai kuwa Serikali imeendesha na inaendelea kuhakiki vyeti vya elimu na baadhi ya watumishi wameshakumbwa na adhabu au kufukuzwa kazi kwa tatizo la vyeti feki.

Mpashaji mwingine aliiambia Mwananchi kuwa, Waziri Mkuu alijibu kuwa Serikali imepokea hoja hiyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Pamoja na kelele za watu tofauti kueleza uwezekano wa kughushi vyetu, si Baraza la Mitihani (Necta), Polisi wala Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliyojitokeza kuzungumzia suala hilo au kuchukua hatua.