SANAMU ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Nyerere
Square mjini hapa, imepata umaarufu kutokana na watu wengi kutoka maeneo
mbalimbali mchini kufika na kupiga picha za kumbukumbu na sanamu hiyo.
Sanamu hiyo ya Mwalimu Nyerere ambayo Baba wa Taifa ameshika fimbo
mkononi, ipo mjini Dodoma, inatumiwa na watu mbalimbali kupiga picha za
kumbukumbu mbalimbali kutokana na heshima ya kiongozi huyo.
“Watu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa Dodoma na mikoa mingine
wanaofika Dodoma wanakwenda mahali hapo na kupiga picha za kumbukumbu
mbele ya sanamu hiyo ya Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere,” anasema Masoud
Abdallah ambaye ni mpigapicha katika eneo hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Hilda Meada katika
mazungumzo na gazeti hili, alisema eneo la Nyerere Square ambalo ni
maarufu kwa wapigapicha ni miongoni mwa maeneo ambayo CDA imeyakabidhi
kwa manispaa.
“Eneo hilo ambalo lilikuwa likisimamiwa na kufanyiwa ukarabati na
uboreshaji na CDA na sasa limekabidhiwa kwa Manispaa ya Dodoma ambayo
inajipanga kuhakikisha eneo hilo na mengine yaliyopo Dodoma yanaboreshwa
na kulingana na mji huu kuwa makao makuu ya serikali,” alisema Maeda.
Alisema manispaa ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha eneo hilo na
maeneo mengine ya wazi yanafanyiwa ukarabati na uboreshaji wa kutosha
ili kuendana na hadhi ya mji.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema manispaa imejipanga kikamilifu
kuhakikisha maeneo yaliyokuwa ya wazi ambayo yamerudishwa kutoka CDA
wanataka kuyaboresha na kuhakikisha yanakuwa sehemu ya vivutio muhimu
kwa watu mbalimbali wanaotembelea likiwamo hilo na Nyerere Square.
Mpigapicha Said Juma alisema, hicho ni kituo chao kutokana na watu
wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini kufika hapo na kutaka kupiga picha
na sanamu ya Baba wa Taifa.
“Hapa kimekuwa kituo chetu cha kupigia picha kutokana na watu wengi
wanaotoka mjini Dodoma, kuja kuweka kumbukumbu ya kuingia hapa kwa
kupigia picha mahali hapa,” alisema Juma.
No comments
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)