Dodoma. Wabunge wa CCM wameitaka Serikali kutoa majibu sahihi bungeni kuhusu utambulisho wa mtu aitwaye Daudi Bashite.
Sakata hilo liliibuka juzi katika kikao cha wabunge wa CCM kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini hapa.
Wabunge tofauti waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa, suala hilo
lilihojiwa kwenye kikao hicho cha ndani ambacho hufanyika kabla ya
mkutano wa Bunge kwa ajili ya kuwekana sawa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao walidai kuwa Serikali imeendesha
na inaendelea kuhakiki vyeti vya elimu na baadhi ya watumishi
wameshakumbwa na adhabu au kufukuzwa kazi kwa tatizo la vyeti feki.
Mpashaji mwingine aliiambia Mwananchi kuwa, Waziri Mkuu alijibu kuwa Serikali imepokea hoja hiyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Pamoja na kelele za watu tofauti kueleza uwezekano wa kughushi vyetu,
si Baraza la Mitihani (Necta), Polisi wala Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliyojitokeza kuzungumzia suala hilo au
kuchukua hatua.
No comments
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)