Nadhan hapa tunapasa kuweka itikadi zetu
za vyama ,dini na kabila pembeni. kuna kipindi tunapaswa kusimama kama
watanzania tukaweka mambo mengine yote mifukoni mwetu tukabaki na
utanzania.
Tanzania ya sasa si tanzania ya
jana...inabadilika inakuja na mambo leo ambayo mengine si mazuri.
Nimemsikia mbunge mmoja akiongea lugha ya ajabu sana bungeni ambayo
sitegemei mbunge msomi na ampambanaji ongee hata kama alikwazika sana.
Angalau kistaarabu angeomba msamaha maana wanasema ada ya mja hunena
uungwana ni vitendo.
Kwa mbunge kutamka maneno "fala"
"mpumbavu" si maneno mazuri ingawa sishangai hili tatizo si kwa wabunge
vijana tu . tulishawah sikia mtu mzima mmoja akiitwa wenzie "wapumbavu"
si maneno ya kistaarabu tukiacha ashakum si matusi. Kuna lugha za
mitaani hizo zisipelekwe bungeni kwa nini wabunge huwa hawapewe semina
ya communication skills? maneno kama "kimenuka" "fala", "wapumbavu"
hatutegemei kuyasikia bungeni.
Wapumbavu wote basi wanapotamkwa
watamkwe pia na huo upumbavu walioufanya au nena wasiishiwe kuitwa
wapumbavu. Nimesikitika sana kwa aina hii ya wabunge ni wapi
tulipokosea sisi watanzania?
Najua bado kuna watu watakuja kutukana
hapa na kumtetea.Kudhihirisha kuwa tuna taifa ambalo either limeathirika
na viroba au matumizi ya bangi lakini sisi wenye akili timamu
hatutanyamaza.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)