Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amepiga marufuku
uuzwaji, uingizwaji wa filamu za nje ambazo hazina stika za TRA ndani
ya mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha amesema baada ya siku kumi ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa
wamekiuka agizo hilo.
Amesema hayo amapema jana ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya
kutembelewa na wasanii wa filamu wakiongozwa na Jacob Stephan
wakilalamikia kuzagaa kwa kazi zao ambazo zimedurufiwa na wafanyabishara
wasiowaaminifu.
Akiongea na waandishi pamoja na wasanii hao, Mh Makonda aliwaagiza watu
wa bodi ya filamu kufanya tadhmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi
yanayouza mikanda ya filamu jiji Dar es Salaam.
Wasanii hao pamoja na wasambazaji walidai hawanufaiki na kazi zao za
filamu kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa
kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridha
yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato.
Wasanii wengine ambao walifika ofisini hapo ni pamoja na Ray Kigosi, Odama, Tino, Jimmy Mafufu pamoja na wasambazaji wa filamu.