MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Tanzania ni moja ya nchi salama kwa uwekezaji Afrika.
Amesema hilo linasababishwa na kutokuwa na matatizo ya migogoro ambayo
inaweza kuhatarisha usalama wa mali za wawekezaji ikilinganishwa na nchi
zingine Afrika.
Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua maonesho ya
kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika Dar es Salaam.
Pia alikaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Ufaransa kuwekeza
katika maeneo mbalimbali hasa kwenye kilimo, nishati, utalii na usafiri
kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.
Makamu wa Rais alisema maonesho hayo ambayo yataambatana na kongamano la
kibiashara la nchi hizo mbili ni fursa ya kipekee kwa wafanyabishara wa
Tanzania na Ufaransa kubadilishana uzoefu katika masuala ya kibiashara
na uwekezaji.
Alieleza kuwa katika kuelekea kwenye uchumi wa viwanda Tanzania haiwezi
kufanya kazi hiyo peke yake, bali kwa kushirikiana na mataifa makubwa
yenye teknolojia ya kisasa katika uwekezaji ikiwamo Ufaransa.
Aliwahakikishia wawekezaji wote wanaokuja nchini kuwa Serikali itafanya
kila linalowezekana kuendelea kujenga mazingira bora kwa ajili ya
uwekezaji.
Alisema ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji
Afrika, Serikali imeendelea kutenga bajeti ya kutosha kuimarisha
miundombinu ya bandari, reli, barabara, usafiri wa anga ili kurahisisha
usafiri na usafirishaji nchini.
Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kongamano hilo
litajikita katika kujadili kwa kina fursa za uwekezaji nchini hasa
kwenye nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano na
miradi ya maendeleo.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram,Mara Kadhaa Mwanadada Mange Kimambi
Amekuwa Akidai kuwa Tanzania si Sehemu Salama kwa Uwekezaji kutokana
na aina ya Serikali Iliyopo hivi sasa.