KIONGOZI Mkuu wa Chama ACT- Wazalendo Zitto Kabwe aunga mkono uteuzi wa
Mshauri wa Chama hicho Professa Kitila Mkumbo uliofanywa na Rais w John
Magufuli.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoituma kwa vyombo vya habari mchana huu akiwa
Dodoma amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa mzalendo kwa kufanya uteuzi
bila kujali itikadi ya Professa Mkumbo
“Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu
Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kw mikono miwili taarifa juu ya uteuzi
wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa
hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na
uzalendo wa kutumikia nchi yetu” ameeleza zitto.
Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea
kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya
Chama ikiwemo Kamati Kuu. Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu
nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu.
Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika
uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu
kama mshauri wa chama. Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo
kwa Taifa utokanao na kila mwananchi, ndio msingi wa kaulimbiu yetu ya
'Taifa Kwanza, Leo na Kesho', hivyo basi tunamtakia kila la kheri ndugu
Kitila katika utumishi wake kwa Taifa letu katika nafasi yake hii mpya.
Wizara Hii ni kubwa na muhimu Sana kwa nchi yetu. Maji ni tatizo moja
kubwa ambalo wananchi wetu wanakumbana nalo na Kama Taifa hatujaweza
kulimaliza. Tunamtakia kila la kheri ndugu Mkumbo katika kuongeza nguvu
kumaliza kero ya maji na kuhakikisha tunaimarisha Kilimo cha Umwagiliaji
nchi nzima. Tunamsihi aanze na ajenda ya Mfuko wa Maji Vijijini na
kuanzishwa Kwa Wakala wa Maji Vijijini utakaosimamia upatikanaji wa Maji
Kwa wananchi wetu.
Kwa hatua hii, tunaona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu Kwa kufanya
kazi na watu wote bila kuwabagua Kwa itikadi zao za vyama. Watanzania ni
wamoja na kauli za kuwagawa zinaumiza zaidi Taifa kuliko kuliweka
pamoja. Tunaamini kuwa Rais Ana nia njema katika uteuzi huu na sisi
tumempa baraka zote Mwanachama wetu mwanzilishi wa Chama kwenda kwenye
nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma. Tunaamini hatamwangusha Rais na
muhimu zaidi hatawaangusha Watanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)