
Leo March 22 jioni, kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars
kilifanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya maandalizi ya
mechi zake mbili za kimataifa dhidi ya Burundi pamoja na Botswana.
Kabla ya kuanza kwa mazoezi, waandishi wa habari waliojitokeza
kushuhudia Stars akifanya mazoezi walipata fursa ya kuzungumza na
nahodha wa Stars Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anakipiga barani Ulaya
kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Waandishi walitaka kujua mambo kadha wa kadha kutoka kwa Samatta ambaye bila shaka nae akafunguka kama ifuatavyo…
Baada ya kufanya vizuri tangu alipojiunga na KRC Genk, kuna offer yoyte rasmi kutoka vilabu vikubwa ambayo imeshamfikia?
Niko pale na nina furaha kuwa pale, kama kuna lolote litatokea ni masuala ya muda tu.
Tanzania imekuwa ikiporomoka kwenye nafasi za viwango vya FIFA, kama nahodha anadhani tatizo liko wapi?
Sio suala la nahodha ni jukumu la wachezaji wote, viongozi na
watanzania. Imefika kipindi tuangalie kwamba tunaelekea wapi, isiwe
wengine wanacheka wakati wachezaji wanaumia, ni suala la watanzania wote
kutengeneza misingi kwa pamoja kwa ajili ya timu ya taifa kwa sababu
inapokuwa inaporoka halafu tunatupiana lawama haipendezi.
Alikuwa anatamani club yake (KRC Genk) ikutane Mnchester United kwenye
robo fainali ya Europa League ili atimize ndoto yake ya kukanyaga Old
Trafford, baada ya ratiba kutoka na timu yake kupangwa na Celta Vigo
amesjisikiaje?
Ni mechi nzuri pia kwa kuongeza uzoefu, sio game ndogo Europa kucheza na Celta Vigo
Baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji bora wa Afrika kwa
wachezaji wa ndani lipewa eneo la kiwanja kama zawadi na wadau nchini
kwa ajili ya kujenga kituo cha soka cha vijana, mpango huo umefikia
wapi?
Siwezi kuanza kujenga kwa sasa kwasababu ntakuja kufa njaa badae,
itafika kipindi kila kitu kitakuwa sawa muda utaongea hilo ni lengo
langu toka kitambo sana na nitalifanya kwa sababu ni lengo ambalo
nilijiwekea mwenyewe.
Kukosekana kwa Thomas Ulimwengu kwenye timu ya taifa kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa kutaiathiri vipi timu ya taifa?
Nitam-miss ni rafikiangu lakini vile vile tulikuwa tumetemngeneza uwiano
mzuri kwe ye timu lakini kama mwanajeshi muda mwingine inabidi
ushirikiane na watu wengine sio lazima awe mtu ambaye umemzoea . najua
hata Tanzania wachezaji wengine na mashabiki pia watam-miss lakini ana
majeruhi na hawezi kutumika inabidi tulielewe hilo.
Maoni yake kuhusu kocha wa taifa wa sasa Salum Mayanga
Alikuwa kocha msaidizi kipindi cha Mart Noij na tulikuwa tunafanya kazi
pamoja kwenye timu ya taifa tunafahamia na anawafahamu wachezaji wengi
wa kitanzania wa timu ya taifa.
Anawasaidiawachezaji wa Tanzania kupata nafasi za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi?
Nashindwa kujibu moja kwa moja kwa sababu kwa sasa naweza kuonekana kama
natafuta sifa ya kuonekana nasaidia wengine nafikiri liachwe labda
wachezaji wanaweza kuongea wenyewe japo hatujafanikiwa kwa kiasi kikubwa
lakini itafika kipindi itakuwa rahisi.
Anajisikiaje pale jina lake linapotajwa na wasanii kwenye nyimbo zao?
Kuna wasanii wengi walikuwa wanataja jina langu kwenye nyimbo zao tangu
nikiwa TP Mazembe labda zilikuwa hazisikiki au watu walikuwa hawatilii
maanani kwa sababu Samatta alikuwa bado yupo Afrika. Najisikia furaha
kwa sababu nahisi watanzania wenzangu wananipa sapoti na wanajali kile
nachofanya , wasanii wote mimi ni washkaji zangu.