Timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo
imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya vijana wenzao wa Burundi
katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Katika mchezo huo ambao Serengeti Boys inautumia kwa ajili ya maandalizi
yao kabla ya kwenda Gabon kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika
kwa vijana chini ya miaka 17, ulishuhudiwa mpaka mapumziko timu hiyo
ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Mabao hayo yalifungwa na Muhsin Makame dakika ya 20 na Nickson Kibabage,
huku Yohana Mkomola akimalizia msumari wa mwisho dakika ya 72 kwa njia
ya mkwaju wa penalti na kukamilisha idadi hiyo ya mabao 3-0.
Baada ya leo kumalizana na Burundi, Jumatatu ijayo kikosi cha Serengeti
Boys kinatarajiwa kucheza mchezo wa mwisho wa kirafiki jijini Dar es
Salaam dhidi ya Ghana kabla ya kwenda Morocco kuweka kambi ya mwisho ya
kujiandaa na michuano hiyo ya vijana.
Katika michuano hiyo itakayoanza kuunguruma Mei 14, mwaka huu, Serengeti
Boys imepangwa Kundi B sambamba na timu za Mali, Niger na Angola. Kama
Serengeti Boys itafanya vizuri kwenye michuano hiyo, basi itajikatia
tiketi ya kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Dunia chini ya miaka 17
itakayofanyika hapo baadaye nchini India.
Tags:
SPORTS AND GAMES
RELATED POSTS
Clouds Tv Wavigeuka Vyombo vya Habari Kuhusu Makonda?, Wamsifia na Kumshukuru
Hatimaye Clouds Fm Kupitia Kipin ...