Mchezaji wa klabu ya Arsenal ambaye hucheza nafasi ya beki wa kulia
Hector Bellerin ameiambia klabu ya Barcelona kuwa yupo tayari kutua Camp
Nou majira ya joto imeripoti redio ya La Graderia.Inasemekena Bellerin alifanya mkutano wa siri na mkurugenzi wa michezo wa Barca Robert Fernandez kuijuza klabu yake hiyo ya zamani kwamba yupo tayari.