March 31 2017 kupitia kipindi cha The weekend chat show Msanii wa Bongo fleva Linah Sanga amekiri alishawahi kutoa mimba takribani mbili kabla ya hii aliyonayo sasa hivi na anategemea kujifungua hivi karibu.
Linah
amesema anajutia hilo na sababu iliyompelekea kutoa mimba hizo ni kwa
sababu alikuwa anamuhofia baba yake kwakuwa hakuwa ameolewa na kudai
baba yake alisha watahadharisha juu ya kubeba mimba wakiwa nje ya ndoa
wajitenge wenyewe kwenye familia yao.
Mtangazaji Soudy Brown alimuuliza Linah kama alishawai kutoa Mimba na majibu yake yalikuwa haya..>>>“Yah
nisiwe muongo nilishawahi kutoa mimba kipindi cha nyuma, nilikuwa
naogopa kwasababu Baba yangu alikataa mtu kubeba mimba nje ya ndoa”
“Mimba nimezitoa, siyo mara nyingi ila naweza kusema kama mara mbilii”:-Linah
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)