Madaktari nchini Kenya, wamefanikiwa kuishawishi mahakama nchini humo kuzuia kuajiriwa kwa madaktari 500 kutoka Tanzania.
Madaktari hao walienda mahakamani kuizuia serikali ya nchi hiyo kutoa
ajira hizo wakidai kuwa kuna madaktari 1,400 wasio na ajira nchini humo.
Wamelalamika kuwa itakuwa ni ufujaji wa fedha kuwa na madakrari 500 wa
Kitanzania watakaolipwa tshs 360,000 kwa siku. Mahakama ya kazi imetoa
agizo hilo Ijumaa jii (March 31), ikisema kuwa litadumu hadi ombi la
maofisa wa afya litakaposikilizwa na kuchambuliwa.
“That leave is hereby granted…to quash the decision of the government…to
hire foreign doctors to be deployed to Kenya,” zimesema nyaraka za
mahakama za March 31.
Mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa serikali kuwajibu maofisa hao na suala hilo litatajwa April 19.
Mwezi huu Rais Dkt John Magufuli alisema kuwa Tanzania itapeleka
madaktari 500 kukabiliana na uhaba uliopo na tangazo la nafasi hizo
lilitolewa kuwataka wenye sifa kutuma maombi. Hata hivyo mpango huo
umepingwa vikali na baadhi ya viongozi wa nchini humo akiwemo Raila
Odinga, ambaye ni rafiki wa karibu na Rais Magufuli.