Siku kadhaa zilizopita staa wa Bongo Fleva Harmorapa aliweka wazi kumzimia staa wa Bongo movies Wema Sepetu baada ya kudai anaweza kumgharamia kwa kila kitu na baadaye April 5 2017 Wema Sepetu kupitia Instagram alimtaka Harmorapa aache kujinadi na asiiharibu image yake.
Sasa leo April 7 2017 baada ya kumfikia ujumbe kutoka kwa Wema Sepetu akionywa kuhusu wazo lake hilo, Harmorapa ameongea na millardayo.com na AyoTV Entertainment alivyoupokea ujumbe huo.
>>”Unajua kwamba hata unapotongoza ama unapoomba kitu kuna mawili; kuna kukubalika na kukataliwa. Kwa hiyo yeye alichokiongea tayari kishaongea. Kwa hiyo haina haja sana kulijadili kwa sababu ameshaongea.” – Harmorapa.

No comments