
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake ,Waziri Mkuu wa
Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn,aliyewasili hivi punde katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar Es Salaam.

Waziri
Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akipewa maua ikiwa ni ishara
ya kumkaribisha kwa upendo nchini Tanzania,mara baada kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mchana,na
baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli,Waziri
Mkuu...

Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye ndege
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere
mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John
Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa
Kitaifa.
Imeelezwa kuwa ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia ni
pamoja na kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na
Ethiopia pamoja na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo
mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.
Mhe. Dessalegn atakutana
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli kwa mazungumzo na kushuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya
ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi
wa Habari.