
Hayo yameibuka baada ya ukimya wa takribani miezi saba kwa kikundi hicho bila ya kutoa kazi mpya ya aina yoyote wala kuonekana katika viwanja mbalimbali vya sanaa ndani ya Tanzania.
"Siyo kila siku kwamba utatoa ngoma mpya, unatakiwa muda mwingine utafute hela ya zile ngoma ulizozitoa na kikubwa mwanzo huwa unatafuta ukubwa kisha ukishapata unaanza kutoa ngoma taratibu taratibu siyo kila siku, wiki hata mwezi unataka kutoa ngoma unashinda na nani?, uzuri wa Yamoto wamezaliwa kwa mtu anayejua muziki vizuri hivyo siasa zote nazijua katika sanaa kwa hiyo lazima tupange mipango ya kwenda na kuangalia mashabiki kama tunao". Alisema Fella
Aidha meneja huyo ameweka wazi mipango ya kundi hilo na kusema siku ya Ijumaa wanatarajia kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la 'Basi' ambayo itakuwa inawarudisha tena watoto hao katika ulimwengu wa