Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wataipinga bungeni bajeti
ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwani haina msaada wowote kwa
wananchi wa hali ya chini na wanaamini fedha hizo hazitapatikana kwa
ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.Mbowe amesisitiza mwaka jana wabunge wa kambi ya upinzani walieleza wazi kuwa bajeti ya mwaka huu isingetekelezeka na ndio kilichotokea kwani mpaka sasa asilimia 34 pekee ya pesa zote za maendeleo ndizo zimetolewa.