
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi
anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa
kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai
kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa. Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL)
ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa
Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika...