Makamu wa Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Godwin
Ngwilimi amekamatwa na polisi huko mkoani Shinyanga na anashikiliwa
katika kituo kikuu cha polisi mkoani humo.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa TLS Mhe.Tundu Lissu ni kwamba Ngwilimi
akiwa katika gari yake alisimamishwa na askari aliyekua kavaa kiraia,
akitaka kukagua gari yake.
Ngwilimi alimtaka Askari huyo ajitambulishe kwanza kwa kutoa
kitambulisho cha kazi kabla ya upekuzi. Lakini badala ya kujitambulisha
alimzuia Ngwilimi na kumuelekeza kituo kikuu cha polisi Shinyanga ambapo
anashikiliwa hadi sasa.